Posts

UFAFANUZI WA KITABU CHA DANIEL NA UFUNUO

THE VOICE OF GOD (prophet paul salim) Prophetpaul78@gmail.com Nimelipenda hilisomo nikaona nilinukuu nikuweke hapa  DANIELI NA UFUNUO   MAELEZO YA SOMO:  Kozi hii ya Danieli na Ufunuo imegawanyika katika sehemu kuu mbili: - Kitabu cha Danieli na kitabu cha Ufunuo.  Katika Kitabu cha Danieli kutoka sura ya 1 hadi ya 6 tutaona maisha ya Danieli na rafiki zake akiwa Babeli chini ya utawala wa mfalme Nebukadneza, Belshaza na mfalme Dario Mmedi.  Katika sura ya 7 hadi ya 12 tutapitia na kujua tafsiri za maono na ndoto alizopewa Danieli. Katika Kitabu cha Ufunuo tutaona mambo aliyoyaona Yohana yaani utukufu wa Yesu Kristo.  Mambo yaliyomo yanayohusiana na makanisa saba ya Asia, na yale yatakayokuwepo baadaye (4 - 22) MALENGO YA JUMLA KWA WANAFUNZI: Kumpatia ufahamu mwanafunzi ili ajue yaliyomo katika Vitabu hivi. Kuleta mabadiliko ya kiroho kwa mwanafunzi ili amche Mungu katika utakatifu. Kumfanya na kumhimiza mwanafunzi kuhubiri Injili ya Kristo kwani muda umeb...